Unajua nini kuhusu chanjo za watoto?
Huwa tunabeba tu malaika wetu clinic tu kufuata ratiba iliyopo kwenye
kadi zao. Kama siku hiyo ni kudungwa sindano haya, kama ni matone twende, na
kuambiana mpe panadol kabla ya chanjo (zile za sindano) ili asipate homa, mara
umwekee barafu…yes nimefanya yote hayo, ila sijui kama kuna ukweli kiasi gani
kuhusu panadol na barafu. Pia sijui kama wote tunajua kazi ya hizo chanjo na
zinafanyaje kazi.
Chanjo ni
nini?
Chanjo
ziliyotengenezwa ili kulinda mpewa chanjo (anaweza hata akawa mtu mzima kama
chanjo ya manjano) dhidi ya ugonjwa fulani. Chanjo ni moja ya vitu muhimu sana
katika makuzi ya watoto.
Chanjo
zinafanyaje kazi?
Chanjo ni
wale wale wadudu wanaoleta ugonjwa huo, wanaingizwa mwilini wakiwa labda
wamepunguzwa makali au wameuliwa fulani hivi, so mfano chanjo ya polio, ni
walewale wadudu wa polio wanaingizwa mwilini wakiwa wamepunguzwa makali.
Wadudu hao
wakishaingia mwilini, mwili wako unatengeneza antibodies dhidi ya ugonjwa
unaosababishwa na wadudu hao.
Hizo
antibodies zikishatengenezwa huwa zinabaki, kiasi kwamba huo ugonjwa ukiingia
au ukilipuka hauwezi kumwathiri mtu ambaye tayari alishachanjwa, maana antibody
zile zilozokwishatengenezwa kwa kutumia wadudu dhaifu zinawashughulikia hao
wadudu wa ukweli.
So chanjo ni
muhimu sana, maana zinamhakikishia mtu kinga ya magonjwa mbalimbali most of the
time kwa maisha yake yote. Magonjwa hayo mara nyingi huwa ni makali, mengine
hayana dawa, so ukiwa hujachanjwa ukikupata ni balaa. Pia magonjwa mengine
yamepotea nchi fulanifulani, kama polio Tanzania inaelekea kupotea kwa sababu
ya kuzingatia sana chanjo.
Na mengine
hatuyaoni sasa hivi kwa sababu karibu watu wote wanachanjwa wakiwa wadogo, so
mlipuko utoke wapi, labda uje na mtu wa nchi nyingine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni