Jumatatu, 31 Machi 2014

Mnyakaya Utangulizi


Habari wapendwa, karibuni katika blog mpya ya MNYAKAYA ambayo imejikita zaidi katika kuzungumzia  mabadiliko katika maisha, ikiwa ni pamoja na matukio mbalimbali yanayo tokea kila siku.

Mnyakaya ni neno lenye asili ya lugha/kabila la wagogo lenye maana ya mwenyenyumba. Kabila hili linapatikana/asili yake ni mkoani Dodoma.

Sababu kuu ya kuipa jina hili ni kwamba katika familia mwenye nyumba ndiye mtu pekee anye fahamu mpangilio, mabadiliko na hata maendeleo ya watoto na familia nzima kwa ujumla.

Pia, ndani ya mnyakaya utapata fursa ya kujifunza ama kujua mabadiliko ya kibinadamu katika nyanja tofauti tofauti katika uwezo wa kufikiri na maamuzi kwa yale anayo yatenda.

Sambamba na hayo yote utapata kujua matokeo ya maamuzi ambayo yamekuwa wakiyachukua mara baada ya jambo kutokea, mazuri au mabaya, sahihi au yasiyo sahihi ambayo humfanya ajute au kufuraia maamuzi/ uamuzi huo.

Hata hivyo kama msomaji na mnyakaya unaweza kuto maonia yako kupitia mambo yanayo zungumziwa ndani yake..
Karibuni na tushirikiane kwa pamoja katika kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni