Jumanne, 1 Aprili 2014

ITAMBUE SAIKOLOJIA KATIKA KUISHI NA WATOTO fahamu ni jnsigani watoto walivyo na umuhimu



  Faida/Manufaa ya Kuwa karibu na Watoto:

  http://tollyzkitchen.files.wordpress.com/2013/03/ready.jpg          Yako manufaa na faida nyingi kwa sisi kuwa karibu na watoto.
Watoto wanaweza kukufanya kuhisi umuhimu fulani na kuhitajika wakati wote na wao.  Mara zote hukubali madhaifu yetu na kuyashangilia yale wanayoyapenda kutoka kwetu.

Ni watu wa kusamehe kwa urahisi sana, kamwe hawawezi kuficha wanachofikiri au kukihisi, uwazi wao huu ni faida kwetu ingawa mara nyingine watu wazima wengine hukasirika.  Ukweli ni kwamba uwazi wao kwetu haumaanishi kutuumiza au kutuumbua.

Ni faida kubwa kwetu pale tunapoona ukaribu wetu na mtoto au watoto fulani unabadilisha maisha au tabia zao.  Kupitia jitihada zako watoto wanaweza kujifunza kujitegemea, ushirikiano, mambo ya afya, kupendana n.k.

Watoto wa leo wengi wanaishi au kupitia katika familia zenye mazingira magumu sana, mfano: Familia zenye ulevi, unyanyasani, talaka na kutengana, matatizo ya kiuchumi.  Watoto hawa wanahitaji kutiwa moyo kuliko wale wenye hali njema.  Utajisikia faraja sana pale utakaposaidia kwa namna moja au nyingine mtoto mmoja kuifikia hatima yake vema.

Kuwa karibu na watoto hutuwezesha kubakia ujana hasa katika fikra zetu.  Hali ya kuutazama ulimwengu na maisha kama mtoto anavyotazama hutupa kupunguza au kuondokana na misongo ya mawazo ya maisha.  Tunajikuta tunafurahia kila kitu kama vile watoto wafanyavyo, hapa tunasema “Yatazame maisha katika jicho la mtoto”.

Kwa kuwa karibu na watoto tunapata nafasi ya kutambua vipawa vyetu, hasa vile vilivyojificha na kuviweka katika utendaji kwa manufaa ya watoto, sisi wenyewe, na jamii nzima kwa ujumla.

Hata kama ukaribu na watoto ilikuwa ni ngumu kwako, taratibu utakapojaribu itafukua upendo wa kweli toka moyoni mwako na mara utatamani kuwa karibu na kujifunza kutoka kwao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni