Jumamosi, 26 Aprili 2014

MTINDIO WA UBONGO NA ULEMAVU WA AKILI KWA WATOTO

Mambo mengi yamesemwa kuhusu tatizo la mtindio wa ubongo, hali ambayo imekuwa ikisababisha jamii mbalimbali kuwanyapaa na hata kuwabagua watoto wenye tatizo hilo.
Kitaalamu, mtindio wa ubongo unaelezwa kuwa ni hali inayompata mwanadamu kwa ubongo wake kushindwa kufanya kazi katika utaratibu wa kawaida. Kimsingi, ni uwezo wa ubongo kutokukua vizuri na kushindwa kufanya kazi yake katika mazingira yake ya kawaida.

Wataalamu wa afya kutoka sehemu mbalimbali duniani ikiwamo Tanzania wanabainisha kuwa mtu mwenye uwezo mdogo wa kufikiri, si kwamba ana matatizo ya akili ama mtindio wa ubongo.
Mtindio wa ubongo unaweza kusababishwa na hali mbalimbali ikiwamo ubongo kuathirika wakati wa kuzaliwa, na hata maisha ya utoto.

Kumbe, yapo mambo matatu yanayosababisha matatizo kwenye ubongo wa mtoto ambaye hajazaliwa mfano ugonjwa wa down syndrome hujitokeza baada ya matatizo katika vinasaba kutokea ambayo baadhi ya matumizi ya dawa husababisha mabadiliko katika vinasaba kama vile dawa za kunywa, ulevi kupindukia (fetal alcohol syndrome) na kuwa na mwili wenye afya dhaifu (fragile X).

Viasili, wakati mwingine huwa ni matokeo ya mtindio wa ubongo. Hiyo hutokana na asili ya kifamilia kuwa inapotokea mmoja wa wanafamilia wana asili na hali hiyo, basi wengine miongoni mwao watapata.

Mbali na hayo, pia matumizi ya dawa kali anazotumia mama wakati wa ujauzito, matumizi ya dawa za kulevya, pombe, hali ya hewa, au hata ajali husababisha kufikwa na hali hiyo.
Utafiti uliowahi kufanywa katika sehemu mbalimbali, unaonyesha kuwa pombe ina athari kubwa na mbaya hasa kwa kina mama wajawazito na matatizo wanayopata yanafahamika kitaalamu Fetal Alcoholic Syndrome (FAS).

Watoto wengi wanaozaliwa na tatizo hili wanakuwa na nyuso ambazo siyo za kawaida (facial deformities). Kwa mfano, watoto hawa wanaweza kuwa na pua bapa na macho yaliyoingia ndani au kupata matatizo ya kusikia na kutokuwa na uwezo wa kusoma.

Ukweli ni kwamba ni vigumu kwa wazazi kuwatambua watoto wao wenye tatizo hili na mara nyingi ni kwa watoto kabla ya kutimiza miaka kati ya mitatu na minne.
Hata hivyo, dalili zifuatazo zinaashiria kuwa mtoto ana tatizo hili. Kwanza, haonyeshi dalili yoyote ya kulia au anaweza kulia kwa kiasi kidogo, huchelewa kutembea na hata kuongea, haonyeshi kuvutiwa na mazingira yanayomzunguka, kwa maana kwamba hata kama kuna vitu vya kuchezea hawezi kujishughulisha navyo.
 
Pia, ni vigumu sana kufundishika na hata kujifunza kusoma huwa ni kazi ngumu ukilinganisha na watoto wa rika lake, hawezi kula mwenyewe, kuvaa mwenyewe au kujifunza kutumia choo.
Zipo dalili nyingi zinazoweza kujitokeza na mara nyingi zinatambuliwa na madaktari maalum wa watoto.

Mtindio wa ubongo na ulemavu wa akili
Mtaalam wa masuala ya mtindio na ulemavu wa akili, Lightnes Kejo anasema katika mahojiano maalumu kuwa watoto wenye matatizo hayo wako wa aina mbili. Watoto wenye mtindio na ulemavu wa akili.

Anasema kuwa tatizo hilo linazidiana kwa kuwa, wapo watoto wenye ulemavu wa akili na wenye mtindio wa ubongo kwa wakati mmoja na wapo wenye matatizo ya mtindio na wenye ulemavu.
Aina hizo tatu zinatofautiana; mtoto aliyeharibika mota ya ubongo kwa kiasi kikubwa hupatwa na mtindio wa ubongo.

Kama mtoto atakuwa ametindia upande wa kushoto, madhara yataonekana upande wa kulia kwa mtoto kuburuza mguu na mkono kutofanya kazi na hivyo hivyo endapo itatokea kwa upande mwingine.

Wakati mwingine husababisha ugonjwa wa kifafa kwa mtoto.
Tatizo lingine linakuja, ikiwa mota ya fahamu haikuharibika, basi mtoto atapatwa na ulemavu wa viungo.

Mbali na dalili za awali, Kejo anabainisha pia kuwa, mtoto anakuwa na dalili za hali hiyo na wakati mwingine chanzo chake ni uvutaji sigara kwa mama mjamzito.
Hii pia husababisha mtoto kuzaliwa njiti, mtoto kuwa na kichwa kidogo, na kutounga uti wa mgongo. Pia aina ya vyakula anavyokula mama.

Kisababishi kingine cha mtindio wa ubongo, ni pale mama anapochelewa kupata huduma ya uzazi anapofikia hatua ya kujifungua ama wauguzi kushindwa kuchukua hatua za haraka baada ya kubaini njia ya uzazi kushindwa kufunguka na uzazi zaidi ya miaka 35.
 
Hata hivyo, utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Emory cha Atlanta, Marekani katika Kitivo cha Dawa, unabainisha kuwa baadhi ya watoto wenye mtindio wa ubongo wanafundishika.

Inaelezwa pia kwamba, watoto hawa wanaweza kubadilika, iwapo tu watafundishwa kwa makini, utulivu na uvumilivu mkubwa.
Mtu anayemfundisha mtoto wa aina hii hatakiwi kamwe kuwa na hasira, na pia inashauriwa sana kuwapongeza wanapofanya vizuri japo kidogo.

Kejo anasema mwalimu anatakiwa awe mpole na ufundishaji wake usiwe wa haraka haraka, aonyeshe mapenzi kwa mtoto, hapaswi kumkemea hata kama anakosea. “Utakuta mwingine hacheki, au anatoka udenda lakini kama akicheza akili inajitengeneza na inaweza kufikia mate yanakatika na hata kucheka na wakati mwingine hurudi katika hali ya kawaida,” anasema.

Watoto wa aina hii inashauriwa wapewe nafasi ya kujenga urafiki na watoto wenzao wa rika lao.
Awali, watoto wenye matatizo ya akili walikuwa wanatengwa na watoto wenzao katika madarasa, kwa kuwekwa kwenye madarasa maalum.

Siku hizi inashauriwa kuwa watoto hao wachanganywe na wanafunzi wenzao wasio na matatizo ya akili, japo hata kwa nusu siku. Utaratibu huu hujulikana kitaalamu, mainstreaming.
Mbali na hayo, inaelezwa pia kuwa wakati mwingine watoto kabla ya kufikwa na hali hiyo ya ulemavu wa akili, wakati mwingine huzaliwa njiti (premature) ambayo mara nyingi mtoto huwa na udhaifu wa viungo.

Matatizo ya uzazi, na uzazi usio salama hufanya mtoto kuzaliwa kabla ya wakati na hiyo husababisha ulemavu wa akili kwani wakati mwingine ukuaji wa ubongo hauwi katika mazingira ya kawaida.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Save the Children, Steve Thorn anasema watoto 210,000 huzaliwa kila mwaka na watoto wa kiume ama hufa au kupata ulemavu kwa kuzaliwa kabla ya wakati.

Anasema kwa mwaka jana pekee, watoto wa kiume njiti 114,000 walizaliwa ikilinganisha watoto wa kike 97,000 na kuongeza idadi ya vifo ama wakati mwingine kupatwa na matatizo ya upofu, uziwi na mtindio wa ubongo.
Dk Daphne Austin wa Mtandao wa Kamisheni ya Afya ya Jamii Uingereza anasema hana shaka kuwa watoto njiti hukua vizuri hadi kufikia wiki 23, 24 na 25 lakini wengi wao hupatwa na ulemavu wa viungo na ubongo.

Jumatatu, 14 Aprili 2014

MADHARA YA KUMSUKA MTOTO AU KUMUWEKA DAWA YA NYWELE...


 
MTOTO kisheria ni binadamu yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 18. Maana ya kutambua  hilo inaonekana pale jamii inapozingatia malezi na makuzi sitahili kwake, katika nyanja mbalimbali za maisha ili anapofikia umri unaomuwezesha kuweza kupambanua mambo, ajiweke mbali na hatari nyingi zinazowapata watu kutokana na historia ya malezi na makuzi yao.

Bila shaka kila mtu anatambua umuhimu wa kutunza afya ya binadamu na kwamba jambo hilo hutakiwa kuanza tangu mtoto akiwa tumboni mwa mama yake.

Usafi wa mwili ni miongoni mwa mambo yanayotakiwa kuzingatiwa na kila mtu, kwa kuwa mtoto hawezi kujitunza kazi hiyo hutakiwa kufanywa na mzazi au mlezi huku akimfunza hatua kwa hatua, kwa kuzingatia umri na uwezo wa akili wa mtoto husika.

Usafi wa mwili ni dhana pana kwani unahusisha hata kumkinga mtoto na matumizi ya bidhaa zenye kemikali zenye hatari kwa afya yake ambazo matokeo yake yanaonekana mara baada ya matumizi ya bidhaa hizo au baada ya muda mrefu kupita.

Baadhi ya watu, hususani wanawake wamekuwa na kasumba ya kuwaruhusu au kuwawekea watoto dawa kwenye nywele kwa lengo la kuzifanya ziwe laini. Jambo hili si jema kwani madhara yake ni makubwa ambayo matokea yanaonekana baada ya miaka mingi, tangu muhusika atumie dawa hizo.
  
Dawa nyingi za kulainisha nywele mathalani relaxer zina kemikali ya Zebaki, ambayo wataalamu wa afya wanasema inapotumiwa kwa muda mrefu inaathiri mishipa iliyo kwenye mfumo wa uzazi.

Mfumo wa uzazi unapoathiriwa na kemikali ya Zebaki, mishipa iliyo kwenye mfumo huo inalegea na kusababisha mwamamke husika kushindwa kushika mimba au kushika mimba ambazo uharibika.

Hata kwa mwanawake mwenye umri pevu ambaye bado anahitaji la kupata watoto dawa hizi ni hatari ingawa kwa kiasi kidogo ikilinganishwa na ilivyo kwa mtoto. Ili kuepuka hatari hizo, inashauriwa mtumiaji wa dawa hizo kuzingatia mashari ya matumizi ya dawa hizo hususani muda.

Kwa kawaida inashauriwa mtu mzima kuweka dawa kwenye nywele siyo zaidi ya mara nne ndani ya mwaka mmoja. Unapoweka dawa unatakiwa usirudie mpaka miezi mitatu ipite, tofauti na hivyo unahatarisha afya yako.

Ipo dhana kwamba siku hizi kuna dawa maalumu kwa ajili ya watoto, lakini ikumbukwe kuwa nazo zina kemikali hivyo ili kuzingatia umuhimu wa afya ya mtoto ni bora kuacha kutumia dawa hizo na badala yake kutunza usafi wa mwili na mavazi ya mtoto ili awe na mwonekano nadhifu usiyo na madhara.

Mtoto anaweza kuwa na mwonekano mzuri wa kupendeza akiachwa mwenye katika hali yake ya asili. Wazazi warejee nyendo zao, wakague utekelezaji wa majukumu yao kwa familia hususani yale yanayogusa moja kwa moja malezi wa watoto kusudi madhara yasiyo ya lazima kwa watoto yadhibitiwe.


 
Hakuna mzazi anatakaye furahi mtoto wake akiolewa alafu akakosa mtoto, pia mtoto anapofahamishwa athari za matumizi ya dawa hizo inakuwa vizuri kwa sababu hata ikitokea akalazimika kuishi nje ya wazazi wake ataweza kuepuka matumizi ya dawa hizo, hata akiwa mtu mzima akaamua kuzitumia atazingatia masharti ya matumizi yake.hivyo ni jukumu la wazazi kuchukua hatua za kuhakikisha afya za watoto wao haziathiriwi na mambo yanayoweza kuzuilika.

Siyo vizuri kuiga kila tunaloona bila kufuatilia na kubaini athari zinazoweza kutokea, kabla ya kutumia kitu ni vizuri kufanya utafiti na uamuzi wa kukitumia au kukiacha ufanywe baada ya kupima faida na hasara zake.

Wazazi wengi wamekuwa na tabia ya kuwasuka watoto mitindo mbali mbali wakidhani wanasaidia kuwapendezesha kumbe wanasaidia kukomaza ubongo wa mtoto kwa kuvutwa mishipa ya ngozi ya kichwa hivyo kumfanya mtoto akomae ngozi ya uso kabla y a wakati. Hiyo ni hatari kubwa sana kwa mtoto wako na madhara utayaona katika ukuaji wa mtoto.

Jumatano, 9 Aprili 2014

HISIA ZA WATOTO



Kuelewa hisia za mtoto kadri anavyokuwa
Tunapoongea kuhusu hisia kadri mtoto anavyokua tunaangalia uwezo wa mtoto:
  • Kuelewa na kujua hisia zake.
  • Kuangalia kwa makini na kuelewa hisia za wenzake.
  • Kuwa na uwezo wa kukabiliana na hisia zake.
  • Kuweza kuamua tabia yake.
  • Kuelewa na kuhisi matatizo ya wenzake.
  • Kuwa na uhusiano nzuri na marafiki, familia na wengineo.
Kadri mtoto anapozaliwa huwa na wepesi wa kukuwa kimawazo na uwezo wa kukabiliana na hali tofauti za hisia.

Kukabiliana na Hisia
Uwezo wa mtoto kukabiliana na hisia ni jambo muhimu katika maisha ya utotoni, hivyo basi mahitaji uwepo wa mzazi.
Mtoto anapozaliwa bado huwa hana uwezo wa wa kukabliliana na hisia zake, ni rahisi kwa mtoto kuzidiwa na hisia na kutoweza kujituliza, hivyo basi anahitaji mwongozo wa mzazi. Ni rahisi mtoto kuwa na hasira kwa sababu wangependa kufanya jambo fulani lakini hawawezi kuifanya hadi kiwango Fulani.
Hisia na tabia zinaligana, kukosa kukabiliana na hisia kwa nji bora, inaweza kuaadhiri uwezo wa mtoto wa kufikiria na kufanya mtoto kukabiliana na hisia zake bila kufikiria.
Wakati mtoto anopoanza shule, tayari huwa na uwezo wa kuelewa hisia zake na tabia za wenzake. Pia huwa na uwezo wa kulinganisha mawazo na hisia kwa kutumia maneno. Hivyo basi kuwa na uwezo wa kubadilisha na kurekebisha hisia zao. Watoto wana uwezo wa kubadilisha na kuzoea hisia zao na kuwa na hali nzuri ya kukabiliana na changamoto vyema, na kuweza kujituliza vizuri.


Uhusiano ni muhimu katika hisia za watoto
Jinsi wazazi wanavyokabiliana na watoto ni muhimu sana katika hisia za mtoto. Uhusiano kati ya mzazi na watoto huwa na adhari katika hisia za mtoto.
Watoto huwa na uwezo wa kukabiliana na hisia kwa kuangalia jinsi watu wa familia wanavyokabiliana na hisia zao. Mzazi huwa kiungo muhimu kwa kumpa mtoto mbinu za kukabiliana na hisia mzito.
Watoto wanahitaji usaidizi na mazoezi katika kukabiliana na hisia zao.


Kusaidia kujenga hisia za mtoto.
Weka mazingira ya nyumba kuwa tulivu naya kuridhisha.
Kubali hisia za mtoto na kuzishugulikia.
Wasomee hadithi zenye hisia tofauti, hii inasaidia mtoto kuelewa zaidi kuhusu hisia zake mwenyewe.
Fundisha mtoto kujieleza kwa kutumia maneno. Mfano, “yaonekana kama huna raha”.
Jaribu kujua hali zinazofanya mtoto kuwa na wasiwasi, raha, hasira au hofu.
Msifu mtoto anapokuwa mtulivu na tabia njema.
Fundisha mtoto kujua tofauti ya hisia na maadili. Mfano, wakati mto amepandwa na hasira, unaweza kumwambia “Najua una hasira lakina sio vizuri kutoa hizo hasira”.
Fundisha mtoto kujua tofauti ya hisia zake na za watu wengine. Mfano, wakati amehuzunika unaweza kumwambia ‘Hivi sasa najua una huzuni lakini unafanya ndugu zako kuwa na huzuni.

Jumanne, 8 Aprili 2014

HATUA ZA UKUAJI WA MTOTO NA KUFIKA UTU UZIMA.

Ukuaji wa binadamu ni safari ya kutoka utotoni kuelekea utu uzima.
Unadai tujipokee tulivyo, pamoja na mema na mapungufu yetu, tukimshukuru Mungu kwamba anatupenda tulivyo.Lakini ni lazima pia tupambane na mapungufu yetu ili kustawisha mema tuliyojaliwa na kufikia uhuru wa ndani.

Kukua kiutu kweli ni kuwajibika maishani kadiri ya mpango wa Mungu aliyetuumba.
Safari hiyo ina hatua mbalimbali, ambazo kila mojawapo ina kazi yake maalumu na ugumu wake.
Kazi hiyo ifanyike katika mazingira ya kufaa, la sivyo tutadumaa.

Kadiri ya Erikson kuna hatua nane zinazofuatana:
1. Mtoto mchanga (miaka 0-2) 2. Mtoto aliyeachishwa (2-4) 3. Chekechea (4-7) 4. Mwanafunzi wa shule ya msingi (7-13) 5. Kijana (13-20) 6. Mtu mzima (20-35) 7. Mtu wa makamo (35-60) 8. Mzee (60 n.k.)

Hatua za kwanza ni fupi lakini muhimu sana, kwa sababu mambo yanayotokea wakati huo yanaathiri maisha yote. Mtoto akisaidiwa vizuri atakuwa mtu ambaye anajisikia salama, anaona mazingira kwa utulivu, anajitawala, anajiamini, haogopi kuwajibika na kuanzisha mambo.

Katika hatua nne za kwanza mtu anahitaji kuziba mapengo yake, katika zile nne za mwisho anahitaji kustawi.
Katika kila hatua hana budi kufanya kazi fulani na kukabili ugumu maalumu ili kukua. Vilevile anahitaji kusaidiwa kufanya hivyo (ndiyo malezi).
Tunapitia hatua hizohizo kila tunapoingia maisha mapya (k.mf. shuleni)

Kujiamini na kuamini wengine

Mtoto anapozaliwa anaanza kuishi katika ulimwengu tofauti na ule aliouzoea tumboni mwa mama. Yuko kwenye hewa na mwanga badala ya kuogelea katika majimaji. Anapaswa kupumua na kutafuta mahitaji yake mwenyewe, ingawa bado anamtegemea sana mama (kwa maziwa, upendo, usalama n.k.).

Ugumu wa kipindi hicho ni kwamba anataka kuwa naye daima, lakini wao ni watu wawili tofauti. Hivyo anapaswa kukubali ukweli huo na kuanza kujiamini. Anaanza kutambua kama anapendwa na kupokewa au la, naye anaanza kutofautisha watu wa kuwaamini na wale ambao asiwaamini.
Anahitaji upendo, usalama na chakula toka kwa mama.

Kujitawala na kuongozwa

Mtoto wa miaka 2-4 anatembea, anasema, anacheza na kuvumbua vitu vingi, anaanza kujitambua na kutambua uhusiano wake na ndugu. Anaanza kutumia utashi ili kujitawala: miaka hiyo anasema mara nyingi, “hapana” na kugongana na mzazi.

Ugumu ni kufaulu kujitawala; akishindwa atakuwa daima na aibu na shaka, hasa akilaumiwa na kupewa adhabu kali mno.

Anahitaji kupokewa na kusaidiwa akuze mema anayoyafanya. Anahitaji pia unyofu na msimamo wa nidhamu kutoka kwa wazazi. Ikiwezekana wamueleze kwa ufupi lakini wazi sababu za kumkataza. Pengine anahitaji kuvumiliwa.

Kuanzisha mambo

Mtoto wa miaka 4-7 anawaza sana kwa ubunifu. Ndio wakati wa kuuliza maswali mengi, “Kwa nini...?”. Anafyonza na kuiga lolote lile. Anaanza kutambua tofauti za jinsia, na mwenendo unaomfaa kama mtoto wa kiume au wa kike.

Ugumu ni kwamba asipojibiwa maswali atajisikia kutupwa. Hivyo ni rahisi kuwa atajisikia daima na hatia, hata asipofanya kosa.
Anahitaji kupokewa, kukubaliwa, kujibiwa.

 

 

 Kutenda

Mtoto wa miaka 7-13 anachukua majukumu ya kiadili. Kisha kutofautisha uadilifu na uovu, anachagua kutenda mema au mabaya. Anapanua mawazo, anafanya kazi za mikono, anatengeneza vitu. Pia anajenga uhusiano na wengine, anafanya kazi pamoja nao. Anahisi kuwa anaweza au hawezi. Ni umri mzuri wa kufundishwa dini na kuongozwa kiadili. Kwa kuwa ana mambo mengi ya kufanya, jinsia huwa imelala, kabla haijaamka katika ubalehe. Lakini hiyo inategemea mazingira na malezi.

Ugumu ni kwamba asiposaidiwa sawasawa atakuwa mnyonge daima, atajiona hawezi chochote, au walau si sawa na wengine. Hivyo mazingira yanaweza kumjenga au kumbomoa.
Anahitaji kutiwa moyo (anapenda ukweli na sifa) ajihisi anaweza kufanya kitu, atambue mahitaji ya wengine na kuwasaidia wayapate.

Kujipatia taswira-nafsi

Umri wa miaka 13-20 ni kipindi cha mpito chenye mabadiliko mengi yanayoathiri mwendo mzima wa kijana ili atoke utoto na kuingia utu uzima. Msichana anabalehe mapema kuliko mvulana. Mvulana ana mwamko mkubwa kuliko msichana. Kuna mvuto mkubwa kati yao, hivyo wanahitaji kuongozwa na nidhamu safi (maadili ya unyago). Ni kipindi cha [[vurugu na cha hisi kali (kulia, kucheka n.k.). Akili inapanuka sana na kupenda nadharia; hivyo ni wakati wa kujipatia maarifa.

Ugumu ni kwamba hatambui mahitaji yake halisi (yuko wapi, naye ni nani?), anaogopa (je, atafaulu kuwa mtu mzima?), hajui kutumia hiari yake vizuri, anataka kuishi tofauti na maelekezo ya wazazi ili ajitegemee. Kutokana na hayo anayatilia shaka mafundisho ya dini (ukweli uko wapi?).

Anahitaji kujifahamu na kujipatia msimamo (taswira-nafsi) katika maisha, la sivyo atazama katika vurugu tupu.

Jumamosi, 5 Aprili 2014

HOW TO LIVE WITH A CHILD AND WHAT ARE THEIR LIKES AND DIS LIKES

An adult has certain rights around children which the children and modern adults rather tend to ignore. A good, stable adult with love and tolerance in his heart is about the best therapy a child can have.
The main consideration in raising children is the problem of training them without breaking them. You want to raise your child in such a way that you don’t have to control him, so that he will be in full possession of himself at all times.


  Likes and dis likes of the child 

It all depends on their personal preference. Not all kids like the same things. However, some things that my kids like are:

3 & 4 year old male

Animals- They have liked all animals that they have came in contact with so far. Some of their favorites are dogs, cats, elephants, worms and bugs.

Activities- They like to play with almost any toys including cars, blocks, dolls, guns, balls and any other toy. They like to fingerprint,color, cut and glue things, make play dough and play with it, paint toast, draw, playing in dirt, skating, riding bikes, do puzzles, blow bubbles, draw with chalk, play sports, sing, play on swing sets and in sand boxes, play in/with water, dance and listen to music. They like to pretend play like pretending to be cops and robbers, doctors, teachers, mommy and daddy and lots of other things.

Co lours- They like all different colors especially bright colors.

Girls in that age group that I have been around seem to like the same things with a few exceptions maybe.

5-6 old boys

I've only been around 1 boy of that age so far. He liked the same things that the 3 & 4 year old do. He also liked going for walks in the mountains and woods, playing with action figures.

5-6 year old girls

A lot of the same things as above unless they are really girly. Girly girls like playing with barbies and other dolls, playing with pretend makeup and nail polish, dressing up as princesses and other people. They also like doing some of the things mentioned above like playing with bubbles, jump ropes, playing with toys, reading, music, dancing and playing house, teachers and doctors.

7-10 year old

I don't know a lot about kids this age but I do have two family members within this age range. They like to do the activities mentioned above but would rather play cops and robbers, fire fighters, police officers or cowboys and Indians instead of pretending to be teachers and doctors. They like to go on nature walks, play in the dirt, wrestle, play on swing sets, play video games, watch tv, play with friends, race and many more things. The animals and colors they like depend on personal preference as it does with every age. Young kids tend to like bright colors though.n that depends his good behavior, his health, his sanity

Alhamisi, 3 Aprili 2014

MABO YANAYOWEZA KUBORESHA UKARIBU/ URAFIKI BAINAYETU NA WATOTO




1.         Kuwakubali na kuwapenda watoto (Appreciation)
Ni ngumu kabisa kuwa karibu na watoto na kutafuta kukubalika nao pasipo kwanza kuwakubali.  Mawasiliano yako na wao yanatakiwa kuwa ya kiwango cha juu kuliko yale unayofanya na watu wazima.  Kama ni mzazi, tamani au tafuta kuutumia muda unapokuwa na watoto vizuri.  Wape muda na wewe kadri inavyowezekana.

Shiriki nao katika baadhi ya yale wanayoyafanya.  Washirikishe pia katika yale unayodhani watapenda kuona ukiyafanya.  Usiwaangalie tu au kuwaacha wakutazame ukifanya.  Kumpakata mtoto wakati wa hadithi ni mfano wa kushiriki nae.  Hii hujenga mahusiano mazuri sana kwao.


2.         Kuwa tayari kutumia nguvu zetu au nishati yetu ya mwili kwa ajili yao
Watoto huwa na nishati au nguvu nyingi katika vile wanavyovifanya.  Hali kadhalika mtu anayetamani kuwa karibu nao ni lazima awe tayari kutumia nguvu zake katika kushiriki nao.  Mfano, watapenda kukimbizana, watapenda kuruka, au kutembea haraka na michezo mingine mingi.

3.         Kuwa na hali nzuri ya utu (Sense of humor)
Hali hii huwafanya watoto kukuona wewe ni sawa nao.  Watoto hupenda sana pale unapokuwa tayari kucheka na kuwa na hisia kama walizonazo.
Najua unahitaji muda wa kuwaza juu ya biashara au kazi zako, na watoto nao kwa upande mwingine wanataka muda ambao hutawaza yalio yako bali yaliyo yao tu.

Mara nyingine, watoto hufanya vitu vya kuchekesha, tunachotakiwa ni kucheka nao na sio kuwacheka.  Hii itaepusha kuwaumiza moyo.

4.         Uvumilifu (Patience)
Uvumilivu ni muhimu sana kwa yeyote anayetaka kuwa karibu na watoto.  Watoto hufanya makosa mengi, na pia ni wataratibu katika kufanya mambo maana ujuzi wao bado ni mdogo.  Kwanza ndio wanajifunza kujitawala na kufuata maelekezo na pia wanahitaji kukumbushwa mara kwa mara.  Ni wakati wa kuulizwa maswali mengi na ya marudio, hata yale yasiyo muafaka.

5.         Kuwa na huruma (Compassion)
Huruma kwa watoto huambatana na uvumilivu.  Mtu mwenye huruma ni yule anayetambua pale mwenzake anapokuwa na tatizo au uhitaji na yuko tayari kutoa msaada.  Watoto humwitaji mtu anayewaelewa na kujali mahitaji yao.  Vipo vitu ambavyo vyaweza kuonekana vidogo na vya kawaida kwetu, kumbe kwa watoto ni vikubwa na vyenye kuwaogopesha sana.  Tunategemea huruma na kujali kwako kutaongezeka hasa kwa wale watoto wenye matatizo au uhitaji mkubwa mfano: watoto wenye magonjwa ya kudumu, ulemavu au matatizo ya kifamilia.

6.         Kuwa mtu unayekubali mabadiliko (Be flexible)
Watoto wako tofauti sana na huwezi kuwa tabiri, mara nyingine watataka kitu fulani na mara hubadilika.  Hawana muda wa kufikiri athari au usumbufu wa kubadilika au kubadilisha maamuzi yao.  Kwa sababu ni vigumu kufahamu ni nini kitajiri kwa mtoto baada ya muda mfupi ujao basi ni lazima tuwe tayari kubadilika.  Pasipo hili basi utakuwa na wakati mgumu sana kuwa rafiki wa watoto.

7.         Kuwa Mgunduzi (Be creative)
Mtu mwenye mawazo na fikra za kigunduzi atapata urahisi sana katika kuwa rafiki wa watoto.  Jaribu kuwa mpya kwa watoto kila mara,  sio kila kitu unachofanya kwao kiwe ni kile kile siku zote.  Amsha hamasa yao kwa vitu, mambo au mawazo mapya mawakati wote.  Watoto hawapendi kufanya kitu fulani kwa njia au mfumo uleule kila wakati.

8.         Kuwa mtu wa watu na mpenda watu (Be sociable)
Watoto huwa wanatusoma sana, pale unapojaribu kuwa mwema kwao, kucheka nao na kuwa karibu nao na wakati hauko hivyo kwa wengine ndani au nje ya familia yako unawafanya wasikuelewe na taratibu huanza kukuhofu.
Waruhusu wakuone ukiwa halisi, hususani unapohusiana na wao pamoja na wengine pia.
Wazazi au mzazi anayependa kujitenga na kuwa mpweke hupata shida sana katika kuwafanya watoto kuwa karibu nae.

9.         Maanisha na ujitoe kwao (Be committed)
Wakati unapoamua kufanya kitu na watoto au mtoto, basi maanisha.  Usiwe na vitu vingi wakati mmoja.  Wape nafasi yao na iwe yao peke yao.
Jitoe kufanya vema uwezavyo katika kuhakikisha unawajali na kuwafurahisha watoto.  Watoto pia hufurahi sana pale wanapoona umetoa moyo wako wote kwa ajili yao. Kama umeamua kuanza kitu nao basi malizia, usikiachie katikati.
Kama unajua au kuhisi kwamba hutomaanisha katika lile unalolifanya ukiwa nao basi ni bora uache mpaka pale utakapojiona kuwa utamaanisha.