Jumanne, 1 Aprili 2014

CHANGAMOTO ZA KUWA KARIBU NA WATOTO




 Kama tunavyo fahamu kuwa watoto ni zawadi kutoka kwa mungu, watoto wamekuwa wakipelekea kuwapo kwa changamoto mbalimbali..
    
Changamoto Zilizopo:
·      Kwa wengi, inaonekana kabisa kuwa, kuwa karibu na watoto mara nyingi huchosha hisia, akili, mwili na hata kusababisha msongo wa mawazo mara nyingine.  Hii huwa ngumu zaidi pale ambapo huna upendo wa dhati kwa watoto.
                                                       
·      Baadhi ya mahitaji au misaada ambayo hatuna budi kuifanya tunapokuwa na watoto hutupa changamoto na wengine huona ni kinyaa au uchafu.

·      Mara nyingine yaweza kuwa rahisi kuambukiza baadhi ya magonjwa madogo madogo kama mafua, kikohozi, ndui n.k. au wewe kuwaambukiza wao pia.

·      Mara nyingine kuwa karibu na wato hutugharimu.  Ziko nyakati ambazo watataka kitu ambacho kinahitaji kununuliwa kwa fedha, au waweza kulazimika kutumia muda wako kufanya matakwa yao.

·      Ziko nyakati watoto hupitia magumu katika familia zao na hali hii huweza kuathiri tabia au hisia zao nahii kuwa changamoto kwa yule aliyekaribu nao.  Mfano magonjwa ya muda mrefu kwa mzazi au wazazi, vifo, kutengana kwa wazazi n.k. hivi vyote vyaweza kuathiri hisia na tabia za mtoto.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni