Jumamosi, 31 Mei 2014

USAFI KWA MTOTO MCHANGA.



Namna ya kudumisha usafi kwa mtoto mchanga.
Mtoto mchanga anahitaji usafi wa hali ya juu, kuanzia mwili wake, nguo, mazingira anayokaa hadi yule anaye mhudumia. Sababu ya uchanga wake ni rahisi sana kupata magonjwa mbalimbali kama atakuwa kwenye mazingira yasiyo na usafi wa kutosha.

Hakikisha mwili wake ni msafi kwa kumuogesha angalau mara mbili kwa siku hasa katika sehemu zenye joto, na nguo zake  zifuliwe kila siku kwa maji safi na sabuni.

Unapofua nguo za mtoto  hakikisha hazichanganywi na nguo za watu wazima na ni vyema nepi zikawa zinafuliwa muda mfupi baada ya kuchafuka. 

Haipendezi kuweka nepi chafu kwenye ndoo kwa masaa mengi, kwanza zitaleta harufu mbaya, zitakuwa ngumu kutakata na zitaharibika mapema.
Unapomuogesha mtoto ni vyema ukitumia maji ya uvuguvugu na kamwe usimuache mtoto kwenye beseni la maji bila kumshikilia.

Kuna watoto wengine huwa hawapendi maji na wanalia sana muda wa kuoga, unaweza kuwa unamuimbia na kumchekea wakati unamuogesha ili aweze kuwa mtulivu na kuona kuwa kuoga ni jambo la kufurahisha. 


 


Kumbuka kumbadilisha mtoto nepi mara tu anapojisaidia ili kumuweka katika hali nzuri na kumuepisha na michupuko. Kama unaumia nepi za kutupa (disposable diapers) hakikisha mtoto hakai nayo muda mrefu sana inaweza mletea madhara.

Kitanda cha mtoto kinatakiwa kiwe safi wakati wote na pia chumba anacholala kisiwe na hewa nzito wala vumbi. Watu wote wanaomhudumia mtoto lazima wawe katika hali ya usafi na pia ni vyema kama kucha zikiwa fupi hii itasaidia mikono kuwa safi zaidi. 

Kama unaweza ni vizuri pia nguo za mtoto zikawa zinanyooshwa baada ya kufuliwa na kukauka ili kuua vijidudu na inashauriwa kuepuka kuanika chini nguo za mtoto maana majani mengine yanaweza mdhuru mtoto au wadudu wakatembelea juu ya nguo na baadaye mtoto akadhurika.

Usafi utapunguza magonjwa mengi kwa mtoto wako na kumfanya awe na afya na furaha.

Chukua hatua sasa !.

Ijumaa, 30 Mei 2014

FAHAMU KIPAJI CHA MWANAO




Namna ya kugundu kipaji cha  mtoto

Watoto wenye akili za ziada au wenye vipaji vya ajabu ni watotot ambao, wamejaaliwa kuwa na IQ {Intelligence Quotient} kubwa kuliko kawaida. IQ ni kifaa maalumu kinachotumiaka kupima akili za binadamu.

Kwa kawaida, watoto wa ain hii wanakuwa na uwezo mkubwa katika masomo ya sayansi na hisabati, pia ni wabunifu na wajanja wa kufikiri haraka haraka na kupata majibu kwa njia za ajabu mno.

Ni watoto wenye uwezo mkubwa sana katika uongozi au wanweza kuwa na vipaji tofauti tofauti kama vile muziki, uigizaji na michezo mbalimbali.

NAMNA YA KUTAMBUA VIPAJI.

Kwanza watoto wenye vipaji maalumu , mara nyingi huanza kujibainisha wakiwa na umri wa kuanzia miaka miwili au umri wa miaka wa kuanza masomo ya awali. Wakati mwingine watoto wa aina hiiwhawajibainishi hadi wanapomaliza elimu ya msingi na hii inatokana zaidi na sababu za kibaiolojia .


 


DALILI ZA KUWEZA KUTAMBUA VIPAJI
 
* Huanza kuongea mapema kwa kutengeneza sentensi kwa ufasaha ukilinganisha na watoto wa umri wake.

* Wanakuwa na uwezo wa kupanga vitu kwa mpangilio sahihi kwa kufuata rangi au aina ya vitu.

* Wanakuwa wajuaji wa hesabu kwa kupenda kuhesabu vitu na hata kukokotoa hesabu.

* Wamejaaliwa kuwa na maono au wanweza kusoma hisia za mtu mwingine, kwa mfano mtoto wa aina hii anweza kumwona mama yake anahangaika ktafuta kitu na yeye akajua anatafuta nini na hata kujua mahali kilipo na hivyo kukifuata na kumletea mama yake, pia wanakuwa na uwezo wa kusoma mawazo ya wazazi wao au hata watu wa karibu wanaowazunguka

* Wanavutiwa sana na sanaa au muziki mapema mno na hata kupenda kuchezea vyombo vya muziki kama viko karibu nao.

* Wanakuwa na moyo wa upendo na hurumawakiwa bado ni wadogo wa umri ukilinganisha na watoto wengine wa umri wao

* Wanakuwa na tabia ya kujitegemea zaidi badala ya kuomba msaada kwa kila kitu, kwa kawaida huwa wanjiamini sana, hivyo ni aghalabu sana kuomba msaada kabisa. Huwa wanaamini katika wao.

Dalili za kuwatambua watoto wa aina hii ziko nyingi sana kulingana na mazingira yaliyowazunguka watoto hao.

NANMA YA KUKUZA VIPAJI VYAO.
Watoto wa aina hii wanhitaji mapenzi sawa na watoto wengine kwani wazazi wengine huwa wanashindwa kuwaelewa watoto wa aina hii na hivyo kuwapuuza, kitu mabcho ni hatari sana kwa maendseleo yao. Wazazi wanatakiwa kufahamu kuwa, licha ya watoto hawa kuwa na akili za ziada, pia bado ni watoto kama watoto wengine.

Ila inashauriwa, wazazi kuwatengenezea watoto wa aina hii mazingira mazuri ya kuendeleza vipaji vyao, kwa kuwanunulia vifaa mbalimbali vya kuchezea, kulingana na matakwa ya vipaji vyao. Ikiwezekana kuwatengea vyumba vyao ambavyo watavitumia kufanya mambo yao bila bughuza, pia inashsuriwa kuwa ni vyema kuwasikiliza na kuwatimizia mahitaji yao.

Huko mashuleni nako inashauriwa kuwaandalia vipindi maalum vitakavyoamsha hisia zao, bila kusahau kuwachanganya na wanafunzi wenzao wenye akili za kawaida.

Alhamisi, 29 Mei 2014

MATATIZO YANAYOWEZA KUMFANYA MTOTO ASINYONYE VIZURI



Jukumu la mama katika kumnyonyesha mtoto.

Wakinamama wa kisasa wameibua tabia ya kutotaka kuwanyonyesha watoto wao maziwa ya mama kwa kuhofia kupoteza uhalisia wa matiti yao eti kwa kile kinachoitwa kulegea na hivyo kupoteza umbo lake la awali.

Hali hii imekuwa ikienea kwa kasi katika jamii nyingi na kuchangia kasi ya ongezeko la vifo vya watoto wachanga na watoto kuanzia umri wa miaka miwili hadi mitano.Ingawa hata wale wanawake wengi wanaonyonyesha , hawanyonyeshi inavyotakiwa hali hii inatokana na sababu nyingi kwa mfano desturi ya kulikiza mapema ,kukosa wa kunyonyesha kwa sababu ya kazi nyingi na fikra potofu zinazowafanya wanawake wasinyonyeshe kama vile kuamini mama akiwa mjamzito asinyonyeshe au mtoto akiharisha hatakiwi kunyonyeshwa.

Kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama ni muhimu sana kwa afya bora na ukuaji wake hii inatokana kwamba maziwa ya mama ni chakula kilicho salama na chenye virutubisho vyote ubora wa maziwa ya mama kwa mtoto anapozaliwa hadi kufikia miezi minne chakula chake kikuu ni maziwa ya mama maziwa hayo ndio chakula ambacho pekee bora ambacho mtoto anaweza kupewa.

Ubora wa maziwa ya mama unatokana na maziwa ya mama kuwa ndio mlo pekee salama na wenye virutubisho vyote ,maziwa ya mama yanasaidia kumkinga mtoto asipate magonjwa kama vile kuharisha ,kifua na surua.Maziwa ya mama ni rahisi hayana gharama na yako tayari kwa wakati wowote na isitoshe yana maji ya kutosha kwa mahitaji ya mtoto.

Mama huanza kunyonyesha mtoto mara tu baada ya kuzaliwa maziwa ya mwanzo ni muhimu sana kwasababu yana virutubisho na viini vya kinga ya asili kwa magonjwa na wataalamu wa afya wanasisitiza kuwa maziwa haya yasikamuliwe na kumwagwa kama watu wengine wanavyofikiria kuwa maziwa haya yana madhara kutokana na rangi yake.

Mtoto baada ya kuzaliwa anyonyweshe maziwa asipewe kinywaji cha aina yeyote ,anyonyeshwe maziwa ya mama tu mpaka atakapofikia miezi minne. Wakati wa kunyonyesha mama anatakiwa kuzingatia mambo mengine muhimu anawe mikono na kuosha matiti kabla ya kumnyonyesha mtoto ,anyonyeshe akiwa amekaa ametulia ,amwekee mtoto chuchu yote mdomoni na kumshikiria titi .

Kila wakati mama anaponyonyesha mtoto anyonyeshe matiti yote mawili,amnyonyeshe mtoto mpaka ashibe kabisa,amtoe mtoto hewa kwa kumweka begani na kumsugua taratibu mara baadaya kunyonya.

Kunyonyesha maziwa ya mama kuna faida nyingi kwa mtoto na hata kwa mama mwenyewe kwani kunasababisha maziwa ya mama kutoka hivyo kumwezesha mtoto kuendelea kunyonya na kushiba vizuri,humkinga dhidi ya magonjwa mengi ya hatari,humsaidia mama asipate ujauzito endapo mama hatakuwa anapata siku zake za hedhi hasa katika kipindi cha miezi sita toka ajifungue , kunyonyesha kunazuia matiti kujaa na kuuma ,hurudisha viungo vya uzazi katika hali yake ya kawaida

Matatizo yanayoweza kusababisha mtoto asinyonye vizuri ni pamoja na mtoto kutopakatwa vizuri,chuchu za mama zikiwa na vidonda au fupi na hata kuzimeziba , mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati wake (njiti),mtoto mwenye kilema cha mdomo na lishe duni kwa mama hivyo maziwa hayatoshi.

Tatizo hili huwakuta wakinamama wanaojifungua kwa mara ya kwanza kinachotakiwa mama azivute chuchu mara kwa mara hadi zitakapotoka kiasi cha kutosha kwa upande wa mtoto njiti au mwenye kilema anatakiwa mama amkamulie maziwa kwenye chombo na amnyonyeshe mtoto.Kwa mama mwenye chuchu zenye vidonda asafishe chuchu na amkamulie na ahakikishe kuwa anasafisha chuchu mara kwa mara.







Ijumaa, 23 Mei 2014

NINI CHA KUFANYA MARA TU MTOTO ANAPOLIA.



Hatua anazopaswa kuzichukua Mama mara tu mtoto anapolia.

Kuna vitu ambavyo mzazi unaweza kufanya ili kumpa faraja mtoto wako pindi anapolia. Yawezekana baadhi ya mambo yatakayoshauriwa hapa yasiwasaidie watoto wote, hivyo basi mzazi ama mlezi ni vizuri ukamjua mtoto wako na kufahamu kwa undani ni kitu gani hasa kinachoweza kusaidia kumtuliza.

1. Kumbeba mtoto
Watoto wachanga huonyesha upendeleo fulani wa hisia, kama vile walivyokuwa ndani ya tumbo, hivyo basi unaweza kujaribu kumvingirisha mtoto wako katika blanketi au nguo zozote za kumbebea kama khanga au vitenge ili kuona kama atapenda hali hiyo.

Watoto wengine hawapendi kuvingirishwa kwenye blanketi na hupenda aina nyingine ya kupata faraja kama vile kubebwa. Wapo wazazi wanaopenda kumbeba mtoto kiasi cha kumfanya mtoto asikie mapigo ya moyo, kitendo ambacho humpa faraja sana mtoto.



2. Kumwimbia nyimbo au sauti za kumbembeleza
Akiwa tumboni mwa mama, mara kwa mara mtoto alikuwa akisikia mapigo ya moyo ya mama. Hali hii ndiyo sababu kubwa ya watoto wengi kupendelea kubebwa na mama zao.

Hata hivyo kuna aina nyingine za sauti zinazoweza pia kusaidia kumtuliza mtoto. Mzazi ama mlezi unaweza kujaribu kuweka muziki wa taratibu au kumuimbia mtoto nyimbo za kubembeleza kwa sauti ya chini sana.

Unashauriwa kutokuweka miziki ya haraka au yenye sauti kubwa kwa sababu inaweza kumwondolea hali yake ya utulivu na hivyo kumfanya ashindwe kuacha kulia.

3. Jaribu kumkanda au kumsugua taratibu (masaji)
Kumkanda kanda au kumsugua mtoto taratibu mgongoni au tumboni kunaweza kumsaidia sana kumfariji mtoto. Iwapo inaonekana mtoto anapata tabu wakati wa kubeua au kucheua, jaribu kumlisha akiwa wima zaidi na kila baada ya kumlisha mweke juu ya bega lako na kumsugua taratibu mgongoni ili kumsaidia atoe gesi kwa kubeua.

Baadhi ya watoto ambao wana “colic” wakati mwingine hutulia hasa wanaposuguliwa taratibu tumboni na hii huweza kuwafanya wajisikie vizuri kwa vile huihisi kwamba angalau mzazi ama mlezi unajitahidi kufanya kitu fulani kusaidia kumwondolea shida yake.

4. Mpatie kitu cha kunyonya
Kwa baadhi ya watoto waliozaliwa, haja ya kunyonya ni kubwa sana na hivyo kumpatia chuchu safi iliyotengenezwa kwa ajili hiyo au kidole kisafi cha mama inaweza kuleta faraja kubwa kwao. Kunyonya kutamsababishia mapigo ya moyo wake kuwa katika kiwango chake cha kawaida, kupumzisha tumbo lake, na kutulia.

Ulezi wa watoto wachanga ni kitu kigumu lakini ulezi wa mtoto ambaye hulia mara kwa mara ni ngumu zaidi. Kupata msaada na kuungwa mkono wakati unapohitaji msaada ni muhimu zaidi.

Mzazi hana budi kufahamu kuwa kwa jinsi siku zinavyopita, na kwa kadri mtoto anavyokua, mtoto anajifunza njia mpya ya kuwa na uwezo wa kuwasilisha mahitaji yake na hivyo ni muhimu mzazi naye kujifunza njia hizo ili kumuwezesha kumpatia mtoto mahitaji yake anayohitaji kwa haraka na wakati unaostahili.