Hatua
anazopaswa kuzichukua Mama mara tu mtoto anapolia.
Kuna vitu ambavyo mzazi unaweza kufanya ili
kumpa faraja mtoto wako pindi anapolia. Yawezekana baadhi ya mambo
yatakayoshauriwa hapa yasiwasaidie watoto wote, hivyo basi mzazi ama mlezi ni
vizuri ukamjua mtoto wako na kufahamu kwa undani ni kitu gani hasa kinachoweza
kusaidia kumtuliza.
1. Kumbeba mtoto
Watoto wachanga huonyesha upendeleo fulani wa
hisia, kama vile walivyokuwa ndani ya tumbo, hivyo basi unaweza kujaribu
kumvingirisha mtoto wako katika blanketi au nguo zozote za kumbebea kama khanga
au vitenge ili kuona kama atapenda hali hiyo.
Watoto wengine hawapendi kuvingirishwa kwenye
blanketi na hupenda aina nyingine ya kupata faraja kama vile kubebwa. Wapo
wazazi wanaopenda kumbeba mtoto kiasi cha kumfanya mtoto asikie mapigo ya moyo,
kitendo ambacho humpa faraja sana mtoto.

2. Kumwimbia nyimbo au sauti za kumbembeleza
Akiwa tumboni mwa mama, mara kwa mara mtoto
alikuwa akisikia mapigo ya moyo ya mama. Hali hii ndiyo sababu kubwa ya watoto wengi
kupendelea kubebwa na mama zao.
Hata hivyo kuna aina nyingine za sauti
zinazoweza pia kusaidia kumtuliza mtoto. Mzazi ama mlezi unaweza kujaribu
kuweka muziki wa taratibu au kumuimbia mtoto nyimbo za kubembeleza kwa sauti ya
chini sana.
Unashauriwa kutokuweka miziki ya haraka au
yenye sauti kubwa kwa sababu inaweza kumwondolea hali yake ya utulivu na hivyo
kumfanya ashindwe kuacha kulia.
3. Jaribu kumkanda au kumsugua taratibu (masaji)
Kumkanda kanda au kumsugua mtoto taratibu
mgongoni au tumboni kunaweza kumsaidia sana kumfariji mtoto. Iwapo inaonekana
mtoto anapata tabu wakati wa kubeua au kucheua, jaribu kumlisha akiwa wima
zaidi na kila baada ya kumlisha mweke juu ya bega lako na kumsugua taratibu
mgongoni ili kumsaidia atoe gesi kwa kubeua.
Baadhi ya watoto ambao wana “colic” wakati
mwingine hutulia hasa wanaposuguliwa taratibu tumboni na hii huweza kuwafanya
wajisikie vizuri kwa vile huihisi kwamba angalau mzazi ama mlezi unajitahidi
kufanya kitu fulani kusaidia kumwondolea shida yake.
4. Mpatie kitu cha kunyonya
Kwa baadhi ya watoto waliozaliwa, haja ya
kunyonya ni kubwa sana na hivyo kumpatia chuchu safi iliyotengenezwa kwa ajili
hiyo au kidole kisafi cha mama inaweza kuleta faraja kubwa kwao. Kunyonya
kutamsababishia mapigo ya moyo wake kuwa katika kiwango chake cha kawaida,
kupumzisha tumbo lake, na kutulia.
Ulezi wa watoto wachanga ni kitu kigumu lakini
ulezi wa mtoto ambaye hulia mara kwa mara ni ngumu zaidi. Kupata msaada na
kuungwa mkono wakati unapohitaji msaada ni muhimu zaidi.
Mzazi hana budi kufahamu kuwa kwa jinsi siku
zinavyopita, na kwa kadri mtoto anavyokua, mtoto anajifunza njia mpya ya kuwa
na uwezo wa kuwasilisha mahitaji yake na hivyo ni muhimu mzazi naye kujifunza
njia hizo ili kumuwezesha kumpatia mtoto mahitaji yake anayohitaji kwa haraka
na wakati unaostahili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni