Namna ya kugundu kipaji cha mtoto
Watoto wenye akili za ziada au wenye vipaji vya ajabu ni watotot ambao, wamejaaliwa kuwa na IQ {Intelligence Quotient} kubwa kuliko kawaida. IQ ni kifaa maalumu kinachotumiaka kupima akili za binadamu.
Kwa kawaida, watoto wa ain hii wanakuwa na uwezo mkubwa katika masomo ya sayansi na hisabati, pia ni wabunifu na wajanja wa kufikiri haraka haraka na kupata majibu kwa njia za ajabu mno.
Ni watoto wenye uwezo mkubwa sana katika uongozi au wanweza kuwa na vipaji tofauti tofauti kama vile muziki, uigizaji na michezo mbalimbali.
NAMNA YA KUTAMBUA VIPAJI.
Kwanza watoto wenye vipaji maalumu , mara nyingi huanza kujibainisha wakiwa na umri wa kuanzia miaka miwili au umri wa miaka wa kuanza masomo ya awali. Wakati mwingine watoto wa aina hiiwhawajibainishi hadi wanapomaliza elimu ya msingi na hii inatokana zaidi na sababu za kibaiolojia .

DALILI ZA KUWEZA KUTAMBUA VIPAJI
* Huanza kuongea mapema kwa kutengeneza sentensi kwa ufasaha ukilinganisha na
watoto wa umri wake.
* Wanakuwa na uwezo wa kupanga vitu
kwa mpangilio sahihi kwa kufuata rangi au aina ya vitu.
* Wanakuwa wajuaji wa hesabu kwa
kupenda kuhesabu vitu na hata kukokotoa hesabu.
* Wamejaaliwa kuwa na maono au
wanweza kusoma hisia za mtu mwingine, kwa mfano mtoto wa aina hii anweza
kumwona mama yake anahangaika ktafuta kitu na yeye akajua anatafuta nini na
hata kujua mahali kilipo na hivyo kukifuata na kumletea mama yake, pia wanakuwa
na uwezo wa kusoma mawazo ya wazazi wao au hata watu wa karibu wanaowazunguka
* Wanavutiwa sana na sanaa au muziki
mapema mno na hata kupenda kuchezea vyombo vya muziki kama viko karibu nao.
* Wanakuwa na moyo wa upendo na
hurumawakiwa bado ni wadogo wa umri ukilinganisha na watoto wengine wa umri wao
* Wanakuwa na tabia ya kujitegemea
zaidi badala ya kuomba msaada kwa kila kitu, kwa kawaida huwa wanjiamini sana,
hivyo ni aghalabu sana kuomba msaada kabisa. Huwa wanaamini katika wao.
Dalili za kuwatambua watoto wa aina hii ziko nyingi sana kulingana na mazingira yaliyowazunguka watoto hao.
NANMA YA KUKUZA VIPAJI VYAO.
Watoto wa aina hii wanhitaji mapenzi sawa na watoto wengine kwani wazazi wengine huwa wanashindwa kuwaelewa watoto wa aina hii na hivyo kuwapuuza, kitu mabcho ni hatari sana kwa maendseleo yao. Wazazi wanatakiwa kufahamu kuwa, licha ya watoto hawa kuwa na akili za ziada, pia bado ni watoto kama watoto wengine.
Ila inashauriwa, wazazi kuwatengenezea watoto wa aina hii mazingira mazuri ya kuendeleza vipaji vyao, kwa kuwanunulia vifaa mbalimbali vya kuchezea, kulingana na matakwa ya vipaji vyao. Ikiwezekana kuwatengea vyumba vyao ambavyo watavitumia kufanya mambo yao bila bughuza, pia inashsuriwa kuwa ni vyema kuwasikiliza na kuwatimizia mahitaji yao.
Huko mashuleni nako inashauriwa kuwaandalia vipindi maalum vitakavyoamsha hisia zao, bila kusahau kuwachanganya na wanafunzi wenzao wenye akili za kawaida.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni